Habari na Matukio

Wanafunzi wa Cohort ya Sita Skuli ya Sheria Zanzibar Wafanya Ziara ya Kimasomo Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu Zanzibar

Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu Zanzibar imepokea ugeni wa wanafunzi wa Cohort ya sita mwaka wa masomo 2026/2027 kutoka Skuli ya Sheria Zanzibar (The Law School of Zanzibar),katika ziara ya kimasomo iliyolenga kuwajengea uelewa wa kina kuhusu utunzaji na usimamizi wa nyaraka, hususan nyaraka za kisheria, pamoja na huduma zinazotolewa na Taasisi hiyo. Wanafunzi hao walitembelea Taasisi hiyo wakiwa...

Walimu Wakuu Zanzibar Wajengewa Uwezo wa Usimamizi Bora wa Nyaraka -Wilaya ya Kaskazini B

Suala la utunzaji wa nyaraka si la Zanzibar pekee, bali ni utaratibu muhimu wa kila nchi katika kuwakumbusha wafanya maamuzi na watunga sera umuhimu wa uwepo wa kumbukumbu sahihi. Ameyasema hayo Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu Zanzibar Ndugu Sheha Makame Mussa wakati akizungumza na Walimu wakuuu wa Skuli za Msingi na Sekondari katika mafunzo ya kuwajengea uwezo juu...

Walimu Wakuu Zanzibar Wajengewa Uwezo wa Usimamizi Bora wa Nyaraka- Wilaya ya Kaskazini A

Maendeleo na matukio mbalimbali duniani, yameendelea kuwa kielelezo muhimu kinachoonesha umuhimu wa utunzaji wa nyaraka na kumbukumbu kitaifa na kimataifa kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo. Akizungumza katika mafunzo ya kuwajengea uwezo walimu wakuu wa skuli za msingi na sekondari kuhusu usimamizi bora wa nyaraka na kumbukumbu, Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Taasisi ya Nyaraka na...