Divisheni hii inaongozwa na Mkuu wa Divisheni na ina majukumu yafuatayo:
Majukumu
- Kusimamia na kuweka mfumo bora wa uhifadhi na utunzaji kumbukumbu katika masjala zote za taasisi za umma
- Kutoa usaidizi wa kitaalamu, ushauri na miongozo kuhusu uanzishaji na usimamizi wa mifumo ya kumbukumbu; masjala na vyumba vya kuhifadhia kumbukumbu katika taasisi za umma
- Kuratibu na kusimamia utekelezaji wa ratiba za uhifadhi na utupaji/uharibu wa mapitio mara kwa mara;
- Kutoa mafunzo, semina na warsha kwa watendaji wa masjala, wasimamizi wa kumbukumbu na watumiaji katika taasisi za umma
- Kutoa usaidizi wa kitaalamu, ushauri na miongozo juu ya kumbukumbu tuli katika utumishi wa umma.
- Kusimamia usimamizi wa kumbukumbu tuli katika Kituo
- Kutekeleza kazi za uhamishaji wa kumbukumbu tuli kutoka ofisi za umma kwenda katika Kituo cha Kumbukumbu Tuli cha Taifa;
- Kutoa usaidizi wa kitaalamu, ushauri na miongozo juu ya kumbukumbu tuli katika taasisi za umma.
- Kutayarisha na kufuatilia utekelezaji wa mifumo ya kumbukumbu kwa ajili ya kusimamia taarifa za kumbukumbu tuli/ zilizofungwa.
- Kuratibu na kutoa miongozo/ushauri wa kupunguza mrundikano wa kumbukumbu katika taasisi za umma.
- Kusimamia ukaguzi na kutoa miongozo inayofaa kwa sehemu/majengo yatakayotumika kuhifadhi kumbukumbu tuli katika ofisi za umma.
Divisheni hii inaongozwa na Mkuu wa Divisheni na ina majukumu yafuatayo:
Majukumu
- Kuratibu na kusimamia ufanyaji wa tathmini ya kumbukumbu katika Kituo cha Kumbukumbu Tuli.
- Kutayarisha ratiba za ujumla za uhifadhi na disposes.
- Kusimamia utekelezaji wa ratiba za uhifadhi na utupaji/uharibu wa mapitio mara kwa mara.
- Kuhakikisha kuanzishwa kwa mgawanyo wa makundi utaozingatia ufanisi wa viwango vya usimamizi wa kumbukumbu tuli.
- Kusimamia upokeaji na uhamishaji wa kumbukumbu tuli kutoka taasisi za umma na binafsi kuingia katika Kituo cha Kumbukumbu Tuli cha Taifa.
- Kutayarisha na kufuatilia utekelezaji wa mifumo ya kumbukumbu kwa ajili ya kusimamia taarifa za kumbukumbu tuli/ zilizofungwa.
- Kutoa miongozo na taratibu za kitaalamu kwa watumiaji na wazalishaji wa kumbukumbu kutoka katika taasisi za umma na binafsi.
- Kutoa elimu na kuhamasisha juu ya tathmini na uhamishaji wa kumbukumbu na nyaraka kwa jamii.
- Kuandaa ripoti za utekelelezaji na kuwasilisha kwa Mkuu wa Kituo.
Divisheni hii inaongozwa na Mkuu wa Divisheni na ina majukumu yafuatayo:
Majukumu
- Kupokea kumbukumbu na nyaraka zote katika kituo kwa mujibu wa taratibu za usimamizi wa kumbukumbu;
- Kutoa mafunzo yanayohusiana na uhualishaji wa kumbukumbu na nyaraka;
- Kudhibiti matumizi salama ya uhai wa nyaraka katika ya kielektroniki;
- Kuimarisha uhifadhi wa kumbukumbu na nyaraka katika teknolojia ya kisasa kwa kuingiza nyaraka katika mfumo ya kidijitali wa kuhifadhi kumbukumbu na nyaraka.
- Kutoa miongozo ya utunzaji kumbukumbu za kielektroniki zinazozalishwa katika wizara, idara, taasisi na mashirika ya umma na binafsi.