Habari na Matukio

Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu Zanzibar Yaadhimisha Siku ya Nyaraka Duniani kwa mwaka 2026

Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu Zanzibar imeadhimisha Siku ya Nyaraka Duniani kwaMaonesho yaliolenga kuonesha mchango wa nyaraka katika kuhifadhi na kurithisha maarifa, tamaduni na urithi wa Zanzibar kutoka kizazi kimoja hadi kingine. Katika maadhimisho hayo, Mgeni rasmi na viongozi mbalimbali walipata fursa ya kutembelea mabanda ya maonesho yaliyohusisha Maulid ya Homu, vikundi vya Dhikri...

Maonesho ya Nyaraka za Kisheria Yaibua Uelewa Mpya kwa Jamii

Katika kuadhimisha Juma la Nyaraka , Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu Zanzibar imeandaa maonesho madogo ya nyaraka za kisheria ikiwa ni sehemu ya shughuli za kuadhimisha Juma la Nyaraka Duniani 2026. Akizungumza katika ufunguzi wa maonesho hayo, Mgeni Rasmi, Prof. Mohammed Hafidh, amesema kuwa Taasisi imefanya jambo muhimu kwa kuandaa maonesho hayo yenye lengo la kuitangaza Taasisi kwa jamii na...

PBZ Bank Yatwaa Ubingwa wa Nyaraka Day Cup 2026

Mashindano ya Nyaraka Day Cup 2026 yaliyoandaliwa na Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu Zanzibar kama sehemu ya shamrashamra za kuadhimisha Siku ya Nyaraka Duniani, yamehitimishwa kwa mafanikio baada ya timu ya PBZ Bank kuibuka bingwa wa mashindano hayo. Mashindano hayo yalizinduliwa rasmi katika Viwanja vya Maisara na Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu Zanzibar, Ndugu...