Matangazo

TAASISI YA NYARAKA NA KUMBUKUMBU ZANZIBAR KUADHIMISHA JUMA LA NYARAKA KUELEKEA SIKU YA NYARAKA DUNIANI 2026

Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu Zanzibar inawataarifu wananchi, wadau na taasisi za umma na binafsi kuwa imeandaa maadhimisho ya Siku ya Nyaraka Duniani tarehe 9 Juni 2026. Katika kuadhimisha siku hiyo muhimu, Taasisi imeandaa Juma la Nyaraka litakaloanza tarehe 3 hadi 9 Juni 2026, likiwa na shughuli mbalimbali za elimu, maonesho na burudani zenye lengo la kuhamasisha jamii na taifa juu ya umuhimu wa nyaraka na kumbukumbu katika kulinda historia, utamaduni na urithi unaoendelea kwa maendeleo ya...

Mafunzo ya Usimamizi wa Nyaraka na Kumbukumbu kwa Walimu wakuu .

Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu Zanzibar kupitia kituo cha Kumbukumbu Tuli imeandaa  mafunzo maalum ya Usimamizi wa Nyaraka na  Kumbukumbu kwa Walimu Wakuu wa Skuli za sekondari na msingi za Mkoa wa Kaskazini Unguja. Lengo la Mafunzo Kujenga uelewa na uwezo kwa walimu katika usimamizi bora wa nyaraka na kumbukumbu katika maeneo yao ya kazi ili kuboresha utunzaji wa taarifa. Mafunzo yatafanyika Wilaya ya Kaskazini A – Ofisi ya Elimu Mkwajuni  Wilaya ya Kaskazini B  –  Skuli ya...