Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu Zanzibar kupitia kituo cha Kumbukumbu Tuli imeandaa mafunzo maalum ya Usimamizi wa Nyaraka na Kumbukumbu kwa Walimu Wakuu wa Skuli za sekondari na msingi za Mkoa wa Kaskazini Unguja.
- Lengo la Mafunzo
Kujenga uelewa na uwezo kwa walimu katika usimamizi bora wa nyaraka na kumbukumbu katika maeneo yao ya kazi ili kuboresha utunzaji wa taarifa.
- Mafunzo yatafanyika
- Wilaya ya Kaskazini A – Ofisi ya Elimu Mkwajuni
- Wilaya ya Kaskazini B – Skuli ya Mahonda
- Muda wa Mafunzo
Mafunzo yataanza saa tatu kamili Asubuhi (3:00 Asubuhi)
- Walengwa
Walimu Wakuu wa skuli za Sekondari na msingi za Mkoa wa Kaskazini Unguja.
- Faida za kushiriki
- Kuimarisha mfumo wa usimamizi wa nyaraka na kumbukumbu
- Kuimarisha utendaji wa kazi katika ofsisi
- Kufahamu mbinu bora za usimamizi wa nyaraka na kumbukumbu
Facebook
WhatsApp