TAASISI YA NYARAKA NA KUMBUKUMBU ZANZIBAR KUADHIMISHA JUMA LA NYARAKA KUELEKEA SIKU YA NYARAKA DUNIANI 2026

Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu Zanzibar inawataarifu wananchi, wadau na taasisi za umma na binafsi kuwa imeandaa maadhimisho ya Siku ya Nyaraka Duniani tarehe 9 Juni 2026. Katika kuadhimisha siku hiyo muhimu, Taasisi imeandaa Juma la Nyaraka litakaloanza tarehe 3 hadi 9 Juni 2026, likiwa na shughuli mbalimbali za elimu, maonesho na burudani zenye lengo la kuhamasisha jamii na taifa juu ya umuhimu wa nyaraka na kumbukumbu katika kulinda historia, utamaduni na urithi unaoendelea kwa maendeleo ya taifa. Ratiba ya Matukio Yaliyopangwa Tarehe 2 Juni 2026 – Mkutano na Waandishi wa Habari Kutakuwa na mkutano na waandishi wa habari (Press Conference) utakaoongozwa na Mhe. Saada Mkuya Salum, Waziri wa Nchi, Afisi ya Rais Ikulu. Tarehe 3 Juni 2026 – Jukwaa la Nyaraka Jukwaa hili litawakutanisha wataalamu na wadau kutoka ndani na nje ya taasisi kujadili masuala muhimu yanayohusiana na usimamizi wa nyaraka na kumbukumbu kwa mustakbali wa sasa na baadae. Tarehe 4 Juni 2026 – Ziara za Kijamii Kufanya ziara maalumu za kuwatembelea na kuwafariji wastaafu wa Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu Zanzibar pamoja na watoto yatima katika Kituo cha Kulelea Mayatima (ZASO Children Home) kilichopo Fuoni Mambosasa, Zanzibar. Tarehe 6 – 7, Juni 2026 – Bonanza la Michezo Kutakuwa na bonanza la mchezo wa mpira wa miguu likihusisha timu za Chuo cha Utawala wa Umma (IPA), Hospital ya Tawakal, Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) na wenyeji wa bonanza hilo; Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu. Tarehe 7 Juni 2026 itakuwa ni mpambano wa kutafuta bingwa atakaepata kombe la “Nyaraka Day Cup” kwa kuzikutanisha timu mbili zilizofuzu raundi ya kwanza kuingia fainaliya mchezo huo.   Sambamba na michezo ya watoto itakayopamba bonanza hilo ambapo zawadi mbalimbali kwa washindi na washiriki zitatolewa. Na Mgeni rasmi katika bonaza hilo anatarajiwa kuwa Mhe. Ali Abulghulam Hussein, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, huku mwenyeji wa bonanza akiwa Mhe. Saada Mkuya Salum atakuwepo. Tarehe 8 Juni 2026 – Maonesho ya Nyaraka za Kisheria Kutakuwa na maonesho ya wazi kwa nyaraka za kisheria kwa wanafunzi wa elimu ya juu wannaosomea masuala ya sheria. Maonesho hayo yatakayofanyika katika ukumbi katika Ofisi ya Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu Zanzibar.Miongoni mwa vyuo vitakavyoshiriki ni Skuli ya Sheria Zanzibar, Chuo Kikuu cha Zanzibar(ZU)na Kituo cha Mafunzo ya Sheria na Utafiti (ZLRC). Tarehe 9 Juni 2026 – Kilele cha Siku ya Nyaraka Duniani Kilele cha maadhimisho ya Siku ya Nyaraka Duniani kitafanyika tarehe 9 Juni 2026 ambapo Mhe. Hemed Suleiman Abdallah, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika hizi. Shamrashamra za maadhimisho hayo zitapambwa na: Maonesho maandiko ya Kiislamu na hati za Kiarabu kwa jamii ya Zanzibar. Maonesho ya Maulid ya Homu. Maonesho ya Dhikri. Maonesho ya elimu ya madrasa. Maonesho ya matibabu ya asili. Maonesho ya Vyakula vya asili na tiba kwa jamii. Taasisi inawakaribisha wananchi wote, wadau pamoja na taasisi za umma na binafsi kushiriki katika shamrashamra hizi na kuwa sehemu ya historia, elimu na utamaduni wetu. Karibu tusherehekee pamoja umuhimu wa nyaraka na kumbukumbu kwa maendeleo ya kizazi cha sasa na kijacho. Kiingilio cha Maonesho hayo ni bureeeeeeeeeeeeeeee!!! Facebook WhatsApp