Katika kuadhimisha Juma la Nyaraka , Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu Zanzibar imeandaa Jukwaa la Nyaraka lililowakutanisha wataalamu mbalimbali kujadili nafasi ya nyaraka na kumbukumbu katika kuimarisha uwajibikaji, haki za wananchi na utawala bora.

Jukwaa hilo ni miongoni mwa matukio muhimu ya wiki ya maadhimisho, likilenga kuongeza uelewa kuhusu mchango wa nyaraka katika maendeleo ya jamii.

Jopo la majadiliano liliwahusisha Moza Z. Mohamed -Mkuu wa Idara ya Nyaraka na kumbukumbu, Fuad A. Mohamed – Mkuu Idara ya kumbukumbu tuli, Anwar Yunus Yahya- Mkuu wa kitengo cha sheria pamoja na Afisa kumbukumbu Ndg Zainab Hassan kutoka Alrahma Hospital.

Wataalamu hao wamejadili kwa kina umuhimu wa nyaraka katika utoaji wa ushahidi wa kisheria, kulinda haki za wananchi na kuimarisha uwajibikaji.

Aidha, walisisitiza umuhimu wa kuimarisha mifumo ya usimamizi wa kumbukumbu ili kuhakikisha upatikanaji wa taarifa sahihi na za kuaminika kwa wakati.

MATUKIO KWA PICHA

Muendeshaji wa Jukwaa la nyaraka Ndg Ali kinasa akifunguwa rasmi jukwaa hilo na kuwakaribisha japo la  wataalamu kutoka katika sekta mbali mbali kujadili nafasi ya nyaraka na kumbukumbu katika kuimarisha uwajibikaji , haki za wananchi na utawala bora .

Mkuu wa idara ya Kumbukumbu tuli Ndg Fuad A. Mohamed akitoa maeleze juu ya historia ya nyaraka na kumbukumbu nchini Zanzibar.

Mkuu wa kitengo cha Sheria katika Taasisi ya Nyaraka na kumbukumbu Zanzibar  Ndg Anwar Yunus Yahya akitoa ufafanuzi juu ya sheria inarohusu kutumika kwa nyaraka ya kidigitali kama ushahidi katika kupata haki.

Mkuu wa Idara ya Idara ya usimamizi wa Nyaraka na Kumbukumbu Bi Moza Z. Mohammed akiongelea nafasi ya nyaraka na kumbukumbu katika kuimarisha uwajibikaji na utawala bora.