Kitengo cha Uhusiano
Kitengo cha Uhusiano kina jukumu la kusimamia mawasiliano ya taasisi na umma pamoja na kuimarisha uhusiano wa taasisi na wadau wa ndani na wa kimataifa.
Kitengo hiki kitakuwa na majukumu yafuatayo:
- Kuandaa na kutekeleza mkakati wa mawasiliano wa Taasisi
- Kuratibu uandaaji wa taarifa mbali mbali za Taasisi
- Kutoa taarifa kwa wananchi juu ya Sera, Sheria, Kanuni na Programu zinazotekelezwa na kusimamiwa na Taasisi
- Kuratibu mikutano na utoaji wa taarifa mbali mbali kwa vyombo vya habari
- Kukuza mashirikiano na kukiunganisha Taasisi ya Kumbukumbu na Nyaraka na Taasisi mbali mbali za ndani na nje ya nchi katika kuimarisha huduma za utafiti
- Kufanya majadiliano mbali mbali kwa wananchi na vyombo vya habari kuhusiana na masuala yanayotekelezwa na Taasisi
- Kusimamia masuala mbali mbali ya kiitifaki ya ndani ya Taasisi