Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kina jukumu la kusimamia matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano katika shughuli za taasisi ili kuongeza ufanisi wa utendaji na kuboresha utoaji wa huduma.
Kitengo hiki kitakuwa na majukumu yafuatayo:
- Kusimamia utekelezaji wa sera ya ICT na e-Government
- Kufanya uchambuzi na kubuni mifumo ya Taarifa za Kiteknolojia ya Mawasiliano na kusaidia Taasisi kutoa huduma bora
- Kusaidia Taasisi kuweza kutumia mifumo mingine inayoandaliwa na kutolewa.
- Kuandaa na kutekeleza mkakati wa kiteknolojia ya mawasiliano ndani na nje ya Taasisi
- Kutunza, kutoa ushauri na kuratibu ununuaji wa vifaa mbali mbali vya kiteknolojia
- Kuanzisha, kuratibu na kuelekeza matumizi ya barua pepe katika Taasisi
- Kuanzisha na kuwezesha matumizi ya mtandao kiambo (LAN) na mtandao mpana(WAN)
- Kuandaa na kutunza ‘web-portal’ na mtandao wa Taasisi
- Kutengeneza na kuhakikisha kuwa mfumo wa usalama wa vifaa na mifumo ya kiteknolojia ya mawasiliano inayotumika
- Kuchunguza, kutambua na kupendekeza vifaa na mifumo ya Kiteknolojia inayofaa kwa matumizi ya Taasisi
- Kuanzisha na kutoa mafunzo kwa watumishi juu ya utuamiaji wa mifumo na vifaa vya kiteknolojia