Kitengo cha Ununuzi na Uondoshaji wa Mali
Kitengo cha Ununuzi na Uondoshaji wa Mali kina jukumu la kusimamia michakato yote ya manunuzi ya vifaa na huduma pamoja na uondoshaji wa mali chakavu za taasisi kwa mujibu wa sheria na taratibu za manunuzi ya umma.
Kitengo hiki kitakuwa na majukumu yafuatayo:
- Kusimamia shughuli zote zinazohusiana na ununuzi na uondoshaji wa vifaa chakavu vya Taasisi
- Kuandaa na kutekeleza mpango wa manunuzi wa Taasisi wa kila mwaka na kuandaa taarifa ya utekelezaji wake
- Kufanya tathmini ya uchakavu wa vifaa na samani za ofisi, kuamua mwisho wa matumizi yake na kuvifuta kwenye daftari la mali za Taasisi
- Kutunza kumbukumbu za zabuni za ununuzi
- Kuandaa mikataba ya ununuzi na kuratibu usimamizi wa utekelezaji wake
- Kuratibu, kutunza na kusimamia ununuzi na Usambazaji wa vifaa na huduma mbali mbali za Taasisi
- Kutoa huduma za Sekretarieti ya Bodi ya Zabuni ya Taasisi
- Kununua, kutunza na kusimamia usambazaji wa vifaa na huduma mbali mbali za ofisi