Kitengo cha Ukaguzi wa Hesabu za Ndani
Kitengo cha Ukaguzi wa Hesabu za Ndani kina jukumu la kusimamia mifumo ya udhibiti wa ndani na kuhakikisha kuwa matumizi ya rasilimali za taasisi yanafanyika kwa uwazi, ufanisi na kwa kuzingatia sheria na kanuni za fedha.
Kitengo hiki kitakuwa na majukumu yafuatayo:
- Kuandaa Mipango na Mikakati ya Ukaguzi
- Kufanya ukaguzi wa mapato na matumizi ya fedha pamoja na mali nyengine za Taasisi na kuandaa ripoti
- Kupitia na kujibu hoja za wakaguzi wa nje
- Kufanya mapitio na kutoa taarifa kama menejimenti imezingatia mapendekezo ya taarifa ya ukaguzi wa ndani
- Kufanya ukaguzi wa thamani ya fedha (Value for money)
- Kuandaa ripoti za utekelezaji na kuziwasilisha kwa Mkurugenzi
- Kufanya ukaguzi wa fedha na miradi iliyotekelezwa na Taasisi