Kitengo cha Sheria.
Kitengo cha Sheria kina jukumu la kutoa ushauri wa kisheria katika shughuli zote za Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu Zanzibar na kuhakikisha kuwa utekelezaji wa majukumu ya Taasisi unazingatia sheria, kanuni na taratibu za serikali.
Kitengo hiki kitakuwa na majukumu yafuatayo:
- Kutoa ushauri juu ya masuala yote ya kisheria na kusaidia katika kutoa tafsiri juu ya Sheria na Mikataba mbali mbali ya Taasisi
- Kutunza kumbukumbu zinazohusiana na masuala muhimu ya kisheria
- Kufanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa sheria na taratibu mbali mbali katika Taasisi ili kufikia dhana ya utawala bora
- Kutowa msada wa kisheria kwa watendaji mbalimbali wa Taasisi katika utendaji wao
- Kuiwakilisha Taasisi Mahakamani dhidi ya mashauri mbali mbali yaliofunguliwa