Katika muendelezo utekelezaji wa shughuli za jumaa la nyaraka , Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu Zanzibar imefanya ziara maalumu ya kuwatembelea na kuwafariji wastaafu wa Taasisi pamoja na watoto yatima katika Kituo cha Kulelea Mayatima (ZASO Children Home) kilichopo Fuoni Mambosasa, Zanzibar.
Ziara hizo zilifanyika kwa wastaafu wanne waliotoa mchango mkubwa katika maendeleo ya taasisi. Wastaafu hao ni Bi. Salma Ahmed wa Rahaleo, Bi. Safia Yussuf Himid wa Mpendae na Bi. Mwanakhamis Khamis wa Pangawe pamoja na bwa nyange.
Aidha, watendaji wa Taasisi walitembelea Kituo cha Watoto wenye mazingira maalum ZASO ikiwa ni sehemu ya kuonesha upendo na mshikamano kwa makundi yenye mahitaji maalum katika jamii.
Aidha, watendaji wa Taasisi walipokelewa na mwanzilishi wa kituo hicho, Bw. Abdul Maulid Haji, ambaye alitoa historia fupi ya kuanzishwa kwa kituo hicho mnamo mwaka 2019 kwa lengo la kuhudumia watoto yatima wanaoishi kwenye mazingira maalumu
Alieleza kuwa kituo hicho hutoa huduma za malazi, matibabu, elimu, lishe bora na mazingira salama kwa watoto hao. Kwa sasa kinahudumia watoto 48, wakiwemo wavulana 26 na wasichana 22 wenye umri kati ya miaka 6 hadi 22.
Taasisi ilipata fursa ya kujionea shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na kituo hicho zikiwemo Utoaji wa elimu pamoja na maendelo ya watoto wanaolelewa kituoni hapo.
Kupitia ziara hiyo, Taasisi ilikabidhi zawadi kwa wastaafu wake kwa lengo la kuthamini mchango wao kwa maendeleo ya Taasisi na kuendeleza upendo na mshikamano uliopo. Pia ilitoa msaada wa vifaa mbalimbali kwa watoto wanaolelewa katika Kituo cha ZASO Children Home kama sehemu ya kuonesha ushirikiano wa jamii, upendo na kujali makundi yenye mahitaji maalumu katika jamii.
🗓 04/06/2026
Watendaji wa Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu Zanzibar wakiwa nyumbani kwa Mstaaafu
Afisa wa Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu Zanzibar akikabidhi zawadi kwa mmoja wa wastaafu wa Taasisi wakati wa ziara maalumu ya kuwafariji na kuthamini mchango wao katika maendeleo ya Taasisi
Afisa wa Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu Zanzibar akikabidhi zawadi kwa mmoja wa wastaafu wa Taasisi wakati wa ziara maalumu ya kuwafariji na kuthamini mchango wao katika maendeleo ya Taasisi
mwanzilishi wa kituo cha ZASO Children Home, Bw. Abdul Maulid Haji, akitoa historia fupi ya kuanzishwa kwa kituo.
Watendaji wa Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu Zanzibar wakiungana na watoto wanaolelewa katika Kituo cha ZASO Children Home katika dua maalumu ya pamoja wakati wa ziara ya kijamii iliyofanyika katika Juma la Nyaraka 2026