Suala la utunzaji wa nyaraka si la Zanzibar pekee, bali ni utaratibu muhimu wa kila nchi katika kuwakumbusha wafanya maamuzi na watunga sera umuhimu wa uwepo wa kumbukumbu sahihi.
Ameyasema hayo Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu Zanzibar Ndugu Sheha Makame Mussa wakati akizungumza na Walimu wakuuu wa Skuli za Msingi na Sekondari katika mafunzo ya kuwajengea uwezo juu ya umuhimu wa utunzaji na uhifadhi wa nyaraka na Kumbukumbu huko Mahonda, Wilaya ya Kaskazini B, Unguja
Amesema taasisi ya nyaraka ni kama ubongo, moyo au akili, ambayo huhifadhi siri na kutunza kumbukumbu muhimu katika maisha ya kila kiumbe, hivyo inapaswa kupewa uzito na kuzingatiwa kwa ukubwa wake.
Hivyo, amewataka walimu kuwa makini na kuyachukulia kwa uzito mkubwa mafunzo hayo, kwani wao pia ni wazalishaji wakubwa wa kumbukumbu na nyaraka za kielimu zinazosaidia Wizara ya Elimu na Serikali kwa ujumla katika kuandaa sera, mipango na maendeleo ya sekta hiyo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu, Ndugu Khatib Suleiman Khatib amesema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeendelea kuchukua juhudi za makusudi katika kuhakikisha suala la utunzaji wa nyaraka na kumbukumbu kupitia taasisi husika linapewa kipaumbele kwa jamii.
Ameeleza kuwa suala la utunzaji wa kumbukumbu limezorota na halifahamiki kwa ukubwa wake kwa baadhi ya jamii, hivyo taasisi hiyo imeandaa mafunzo na semina mbalimbali ili kuipa jamii uelewa kuhusu umuhimu wa suala hilo, hususan kwa walimu wakuu wa shule mbalimbali.
Aidha, washiriki waliopatiwa mafunzo hayo wameeleza baadhi ya changamoto wanazokabiliana nazo, zikiwemo kuwepo kwa taarifa zisizo sahihi za wanafunzi kutokana na ukosefu wa nyaraka muhimu kama vyeti vya kuzaliwa. Hata hivyo, waliishukuru Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu kwa kuandaa mafunzo hayo, ambayo yatawajengea uwezo katika uhifadhi na utunzaji bora wa nyaraka.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu Zanzibar Ndg Khatib S. Khatib akitoa maelezo machache na kumkaribisha mgeni rasmi kufungua mafunzo ya kuwajengea uwezo walimu wakuu wa skuli za sekondari na msingi juu ya usimamizi wa nyaraka na kumbukumbu yaliofanyika Skuli ya Mahonda, Wilaya ya Kaskazini B, Unguja
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushari Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu Zanzibar Ndg Sheha Makame Mussa akizungumza na walimu wakuu wa Skuli za msingi na Sekondari wa Wilaya ya Kaskazini B, Unguja wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo juu ya usimamizi wa nyaraka na kumbukumbu.
Walimu wakuu wa Skuli za Msingi na Sekondari wa Wilaya ya Kaskazini B, Unguja walioshiriki katika mafunzo ya usimamizi wa Nyaraka na Kumbukumbu yalioandaliwa na Taasisi ya Nyaraka na Kumbukukumbu Zanzibar yaliofanyika katika Skuli ya Mahonda.
Msaidizi Afisa Kumbukumbu ndg Omar Karume Juma akiwasilisha mada ya usimamizi wa nyaraka na kumbukumbu kwa walimu wakuu wa Skuli za Msingi na Sekondari za Wilaya ya Kaskazini B, Unguja katika mafunzo ya kuwajengea uwezo juu ya usimamizi wa nyaraka na kumbukumbu yaliofanyika Skuli ya Mahonda.
Walimu wakuu wa Skuli za Msingi na Sekondari walioshiriki katika mafunzo ya usimamizi wa Nyaraka na Kumbukumbu wakisikiliza kwa umakini mafunzo yalioandaliwa na Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu Zanzibar.
Mwalimu mkuu Skuli ya Sekondari Fujoni Rukia Ali Salum akitoa maoni kuhusu daftari la usajili wa wanafunzi katika mafunzo ya usimamizi wa Nyaraka na Kumbukumbu yalioandaliwa na Taasisi ya Nyaraka na Kumbukukumbu Zanzibar.
Msaidizi Mwalimu mkuu Skuli ya Bumbwini Msingi Ndg Zahran Salum Kidemea akiuliza swali katika mafunzo ya usimamizi wa Nyaraka na Kumbukumbu yalioandaliwa na Taasisi ya Nyaraka na Kumbukukumbu Zanzibar.
Mwalimu mkuu Skuli ya Sekondari Kitope Bi Jina Ali Afadhali akiuliza swali na kutoa maoni katika mafunzo ya usimamizi wa Nyaraka na Kumbukumbu yalioandaliwa na Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu Zanzibar.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu Zanzibar Ndg Khatib S. Khatib akijibu maswali na kutoa ufafanuzi wa baadhi ya maswali yalioulizwa na washiriki katika mafunzo ya kuwajengea uwezo walimu wakuu wa skuli za Sekondari na Msingi juu ya usimamizi wa nyaraka na kumbukumbu yaliofanyika Skuli ya Mahonda, Wilaya ya Kaskazini B, Unguja.
Picha ya pamoja , mgeni rasmi na washiriki wa mafunzo ya usimamizi wa Nyaraka na Kumbukumbu yalioandaliwa na Taasisi ya Nyaraka na Kumbukukumbu Zanzibar.