Habari na Matukio

MAFUNZO YA UANDAAJI WA DAFTARI LA UHAI WA KUMBUKUMBU

Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu Zanzibar imetoa mafunzo elekezi kuhusu ukusanyaji wa maoni katika uandaaji wa Daftari la Uhai wa Kumbukumbu (Records Retention Schedule) kwa watendaji kutoka Taasisi mbalimbali za umma. Mafunzo hayo ya siku mbili yamefanyika kuanzia tarehe 04 hadi 05 Februari, 2025 katika jingo la Taaisi ya Nyaraka na kumbukumbu Zanzibar, yakilenga kuwajengea uwezo washiriki kuhusu...

TAASISI YA NYARAKA YAADHIMISHA SIKU YA NYARAKA DUNIANI

Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu Zanzibar leo tarehe 9 Juni 2025 imeadhimisha Siku ya Nyaraka Duniani kwa hafla maalum iliyofanyika katika ukumbi wa Zanzibar Ocean View Hotel, Kilimani. Mgeni rasmi katika hafla hio alikua ni Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais – Ikulu, Ndugu Saleh Juma Mussa, akifuatana na Mkurugenzi wa Taasisi, Ndugu Khatib Suleiman Khatib, Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri, Ndugu Sheha...

MAKAMO WA PILI WA RAIS AWEKA JIWE LA MSINGI JENGO JIPYA LA NYARAKA

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imejipanga kufanya mabadiliko na mageuzi makubwa katika Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu kwa lengo la kuongeza ufanisi katika utendaji kazi, hususan katika utunzaji wa nyaraka na kumbukumbu za Taifa. Ameyasema hayo leo jumapili tarehe 28 Disemba 2025 wakati wa uwekaji wa jiwe la...