Kitengo cha Fedha na Uhasibu.
Kitengo cha Fedha na Uhasibu kina jukumu la kusimamia rasilimali za kifedha za taasisi kwa mujibu wa sheria na kanuni za fedha za serikali.
Kitengo hiki kitakuwa na majukumu yafuatayo:
- Kuandaa taarifa za mapato na matumizi kwa kila mwezi, robo mwaka, nusu na mwaka kwa kuzingatia Sheria na Kanuni za Fedha
- Kudhibiti na kusimamia mapato na matumizi ya fedha kulingana na bajeti
- Kutayarisha hati za malipo kwa watumiaji kwa mujibu wa kasma za mgao wa Taasisi
- Kuandaa na kufanya malipo mbali mbali kama yatakavyoidhinishwa na Mkurugenzi
- Kutunza kumbukumbu ya hesabu za Taasisi
- Kuandaa malipo na kuyawasilisha katika mifuko na makato maalumu ya watumishi kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zinazohusika
- Kutayarisha makisio ya matumizi ya kawaida na maendeleo
- Kufuatilia upatikanaji wa fedha zilizotengwa
- Kufanya usuluhisho wa hesabu za Taasisi
- Kujibu hoja zote za ukaguzi zilizoulizwa katika mwaka fedha uliopita