Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu Zanzibar imetoa mafunzo elekezi kuhusu ukusanyaji wa maoni katika uandaaji wa Daftari la Uhai wa Kumbukumbu (Records Retention Schedule) kwa watendaji kutoka Taasisi mbalimbali za umma.
Mafunzo hayo ya siku mbili yamefanyika kuanzia tarehe 04 hadi 05 Februari, 2025 katika jingo la Taaisi ya Nyaraka na kumbukumbu Zanzibar, yakilenga kuwajengea uwezo washiriki kuhusu umuhimu wa upangaji, uhifadhi na uondoaji wa kumbukumbu kwa kuzingatia miongozo na sheria husika. Katika mafunzo hayo, washiriki ambao ni wadau wa sekta ya umma walipata fursa ya kutoa maoni, mapendekezo na uzoefu wao unaohusiana na usimamizi wa nyaraka na kumbukumbu katika taasisi zao.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu Zanzibar, Bw. Khatib Suleiman Khatib alitoa neno la utangulizi na kueleza dhamira ya Taasisi katika kuimarisha usimamizi wa nyaraka na kumbukumbu katika taasisi za umma, kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua mafunzo hayo.
Mgeni rasmi wa mafunzo hayo, Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu Zanzibar, Sheha Makame Mussa, alisisitiza umuhimu wa ushirikiano wa wadau katika mchakato wa uandaaji wa Daftari la Uhai wa Kumbukumbu, akieleza kuwa maoni yatakayokusanywa yatasaidia kuboresha nyaraka hiyo muhimu kwa maslahi ya utawala bora na uhifadhi wa kumbukumbu za taifa.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu Zanzibar Ndg Khatib Suleiman Khatib akitowa maelezo machache kwa washiriki kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufunguwa rasmi mafunzo ya Daftari la uhai (Records Retention Schedule)
Mwenyekiti wa Bodi ya ushauri Ndg Sheha Makame Mussa akitowa maelezo machache kwa washiriki kabla ya kufunguwa rasmi mafunzo ya Daftari la uhai (Records Retention Schedule)
Watendaji wa Taasisi za umma wakisikiliza maelezo machahe kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya ushauri Ndg Sheha Makame Mussa wakati alipofunguwa rasmi mafunzo ya Daftari la uhai (Records Retention Schedule)
Afisa Kumbukumbu Ndugu Abass Bakari Yakoub akiwasilisha mada kuhusu daftari la uhari (Records Retention Schedule) kwa washiriki wa mafunzo hayo yaliofanyika Taasisi ya Nyaraka Kilimani Zanzibar
Washiriki wa mafunzo ya Daftari la Uhai wa Kumbukumbu wakifanya majadiliano juu ya mada iliyowasilishwa
Mkurugenzi Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu Zanzibar Ndg Khatib Suleiman Khatib ,Mwenyekiti wa Bodi Ndg Sheha Makame Mussa wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo ya Daftari la uhai wa Kumbukumbu yalioandaliwa na Taasisi ya Nyaraka.