Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu Zanzibar leo tarehe 9 Juni 2025 imeadhimisha Siku ya Nyaraka Duniani kwa hafla maalum iliyofanyika katika ukumbi wa Zanzibar Ocean View Hotel, Kilimani.

Mgeni rasmi katika hafla hio alikua ni Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais – Ikulu, Ndugu Saleh Juma Mussa, akifuatana na Mkurugenzi wa Taasisi, Ndugu Khatib Suleiman Khatib, Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri, Ndugu Sheha Makame Mussa , pamoja na wageni waalikwa kutoka taasisi mbalimbali.

Maadhimisho ya mwaka huu yamebebwa na kauli mbiu: “Archives are Accessible”, ikilenga kuhamasisha upatikanaji na matumizi ya nyaraka kwa uwazi kwa maendeleo ya kijamii na kitaifa.

Hafla ilijumuisha uwasilishaji wa mada na mijadala kuhusu umuhimu wa nyaraka, pamoja na utoaji wa vyeti vya shukrani kwa waliotoa mchango mkubwa katika sekta hii.

Waliotunukiwa ni Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ), Shirika la Maendeleo la Uturuki TiKA  Mkurugenzi wa Taasisi, Ndugu Khatib Suleiman Khatib, Bi Maryam Olban Ali na Ndugu Makame Mtwana Haji

MATUKIO KWA PICHA

Mkurugenzi wa Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu Zanzibar Ndg Khatib S. Khatibu akitoa maelezo machache juu ya Historia Taasisi ya Nyaraka pamoja na kumkaribisha Katibu Mkuu Ofisi ya Raisi Ikulu ndugu Saleh Mussa Juma kufungua Kongamano  la siku ya Nyaraka Duniani lililofanyika katika ukumbi wa mkutano Ocean View Zanzibar

Mkurugenzi wa Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu Zanzibar Ndg Khatib S. Khatibu akiwasilisha  mada ya umuhimu wa Nyaraka na Kumbukumbu katika Kongamano  la siku ya Nyaraka Duniani lililofanyika katika ukumbi wa mkutano Ocean View Zanzibar

Watendaji wa Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu Zanzibar pamoja na wananchi  wakisikiliza hotuba ya Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais – Ikulu, Ndugu Saleh Juma Mussa,akifungua Kongamano la siku ya Nyaraka Duniani lililofanyika katika ukumbi wa mkutano Ocean View Zanzibar

Ndugu Haji Mdungi Mkufunzi wa Chuo cha Utawala wa Umma IPA akiwasilisha  mada ya umuhimu wa Nyaraka na Kumbukumbu katika Kongamano  la siku ya Nyaraka Duniani lililofanyika katika ukumbi wa mkutano Ocean View Zanzibar

Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais – Ikulu, Ndugu Saleh Juma Mussa,akimtunukia Zawadi Mkurugenzi wa Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu Zanzibar Ndugu Khatib Suleiman Khatibu   kwa kutambua mchango wake mkubwa katika kuimarisha usimamizi wa Nyaraka na kumbukumbu katika Taasisi za Umma.

Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais – Ikulu, Ndugu Saleh Juma Mussa,akiwa katika picha ya pamoja na Watendaji wa Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu Zanzibar mara baada ya kufungua Kongamano la siku ya Nyaraka Duniani lililofanyika katika ukumbi wa mkutano Ocean View Zanzibar