Bodi ya Ushauri wa Nyaraka na Kumbukumbu Zanzibar imefanya ziara ya kikazi  Kisiwani Pemba na kutembelea baadhi za Wizara na Taasisi za umma. Ziara hiyo imeanzia tarehe 14 na 15 Agosti 2025 kwa kutembelea ofisi za Shirika la Meli, Shirika la Bandari, Wizara ya Afya ,Wizara ya Ardhi  pamoja na Kamisheni  ya Ardhi. Katika ziara hiyo bodi imeweza kujionea jinsi kazi za uzalishaji na utunzaji wa Kumbukumbu na Nyaraka unavyofanyika.

Akiiongoza Ziara hiyo Mwenyekiti wa bodi Ndg Sheha Makame Mussa akiambatana na wajumbe Bi Hurina Said Mohamed, Ndg Kombo Gora Haji, Ndg Mussa S.Maftah na Ndg Khatib S.Khatib.Wajumbe wameweza kujionea mafaniki  ikiwemo matumizi ya mfumo wa Ofisi mtandao(e-office) pamoja na changamoto zikiwemo ufinyu wa maeneo ya kuhifadhia nyaraka na kumbukumbu, uhaba wa vifaa vya kuhifadhia nyaraka na changamoto ya huduma ya mtandao, hususan kwa matumizi ya mfumo wa e-office.

Aidha, Mwenyekiti wa Bodi ametoa msisitizo kwa viongozi kuhakikisha vitengo vya kumbukumbu vinapata kipaombele cha kutosha, hususan katika uandaji wa bajeti ambapo mahitaji muhimu ya kitengo yanapaswa kuzingatiwa. Pia amesisitiza kwamba maafisa wa kumbukumbu wanapewa fursa za mafunzo ili kuimarisha uwezo wao wa kitaaluma na kuhakikisha utendaji bora wa huduma za nyaraka na kumbukumbu.

MATUKIO KWA PICHA

Wajumbe wa Bodi wakiongozwa na Mwenyekiti Ndugu Sheha Makame Mussa wakipata maelekezo kutoka kwa Mkurugenzi wa shirika la Bandari Pemba

 Mwenyekiti Ndugu Sheha Makame Mussa akitoa maelekezo kwa  Maafisa watunza Nyaraka na Kumbukumbu katika Afisi ya Shirika la Ardhi Pemba.

 Mwenyekiti Ndugu Sheha Makame Mussa akitoa maelekezo kwa  Maafisa watunza Nyaraka na Kumbukumbu katika Afisi ya Shirika la Nyumba Pemba.